Description
The Pausinystalia Johimbe plant is native to West Africa and has been in use as a medicine for centuries. Yohimbe Bark has multiple uses and it can be used as a remedy for the following: weight management, sexual dysfunction, mental illness and pressure.
Swahili
Mmea wa Yohimbe (Pausinystalia Johimbe), nchini Nigeria ukijulikana kama Yoruba na Duala nchini Cameroon umekuwa ukitumika kama dawa tangu karne nyingi zilizopita. Maganda yake yake yamekuwa yakitumika kwa namna nyingi hususani kudhibiti uzito wa mwili, kushindwa kusimamisha uume na kukosa hamu ya tendo la ndoa, maradhi ya akili pamoja na shinikizo la damu. Mmea huu una asili ya Africa ya magharibi pamoja na Afrika ya kati.
Uchanganuzi wa bidhaa
- Bidhaa inapotokea: Cameroon
- Vidonge 60
- Nzuri kwa watu wote wanaokula tu vyakula vitokanavyo na mimea
- Ni mmea wa Yohimbe kwa 100%
- Huimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa
- Vidonge vinavyoweza kulainika kwa haraka
Madhara yanayoweza kutokea
Haushauriwi kutumia Yohimbe kipindi cha ujauzito.Inaweza kusababisha changamoto kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kufeli kwa figo, kupooza na hata shambulio la moyo. Tafuta msaada wa haraka wa kiafya kwa mtaalamu yeyote aliye karibu nawe ili kujiridhisha ikiwa bidhaa hii inafaa kwa ajili yako.
Faida za kiafya za Yohimbe
- Kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.
- Yohimbe imekuwa ikitumika kama tiba ya tatizo la kutokusimamisha uume vizuri pamoja na ugumba kulingana na ukweli kuwa husaidia kuongeza presha ya damu kwenye uume na hivyo kusaidia uume kusimama kwa muda mrefu.
- Kutibu shinikizo la juu la damu
- Kama mishipa ya damu ni myembamba moyo hulazimisha kusukuma damu na hivyo kuweza kusababisha kuongeza presha ya damu. Yohimbe inaweza kusaidia kuondoa vizingiti vyote na hivyo kusaidia kuimarisha afya ya moyo.
- Yohimbe husaidia kupunguza uzito.
- Hii ni moja ya faida muhimu zaidi ya maganda ya Yohimbe inayofahamika. Alkaloid aina ya Yohimbine, iliyopo kwenye maganda ya Yohimbe,inaweza kuzuia aina Fulani ya adrenoceptors mwilini, kitua ambacho hupelekea kuongezeka kwa kiwango cha norepinephrine mwilini. Norepinephrine kazi yake ni kuondoa mrundikano wa mafuta na husaidia kuvunja vunja mafuta katika sehemu mbalimbali za mwili.
- Hupunguza madhara yatokanayo na tiba za msongo wa mawazo.
- Dawa nyingi za kemikali zinazotumika kutibu matatizo ya msongo wa mawazo na udhoofu huweza kupelekea kuondoa ashk/kiu ya mapenzi. Yohimbe imekuwa mbadala mzuri wa kuzikabili changamoto zitokanayo na Athari ya tiba za aina hii.
- Inaweza kuimarisha afya ya akili
- Yohimbe inaweza kudhibiti kiwango cha Dopamine pamoja na coenzyme NAD kwenye ubongo ambayo kiasili huathiri kwa namna chanya “ari” na “akili”.
Uhifadhi
Weka sehemu kavu isiyokuwa na unyevu.