Description
Pearl millet is a highly nutritious food that is widely grown in Africa and Asia. It is a gluten free grain with a low Glycemic Index which makes it a great option for people with gluten-sensitivity or diabetes.
Product specifications
- Gluten Free
- Rich in fiber
- Stabilizes cholesterol levels
Swahili
Huu ni uwele wa kiasili. Uwele ni moja ya nafaka hai na asili yenye virutubisho vingi muhimu. Zao hili hulimwa kwa wingi Africa na Asia. Ni nafaka isiyo na gundi na ina kiwango cha chini cha Glysemic Index ambayo ni msaada mzuri kwa watu wenye shida ya mmeng’enyo wa chakula au kisukari. Kama ilivyo kwa nafaka zingine uwele una ladha nzuri yenye kuvutia na aghalabu ukipikwa pamoja na mchanganyiko mwingine wa chakula ni rahisi wenyewe kutawala rangi na ladha ya chakula chote. Uwele umekuwa ukitumika kutengenezea chapati, mikate, maandazi, uji wa lishe na ugali kwenye jumuisho la vyakula vyenye afya na muhimu zaidi tangu Nyuma za kale.
Sifa Bainifu za bidhaa
- Hauna gundi
- Una nyuzi nyuzi nyingi
- Huondoa lehemu
- Unakuzwa kiasili
- Lishe bora
- Tumia kabla ya muda wa matumizi
- Imetengenezwa na Kusambazwa na WFN Naturals
Uhifadhi
Weka mahali pasipokuwa na unyevu
Jinsi ya kuandaa
Loweka kwa muda usiopungua saa 12. Osha na maji ya baridi kisha chemsha, katika kila kikombe kimoja cha uwele weka vikombe viwili vya maji. Baada ya kuchemsha kwa kwa dakika tano ipua na acha pishi lako lipoe kwa dakika 30.
Zingatio
Viambata, taarifa za virutubisho vyake na vifungashio vyake vinaweza kubadilika. Maelezo sahihi zaidi yanapatikana kwenye karatasi ya maelekezo ya bidhaa.
Maswali ya Mara kwa Mara (FAQ)
Je, uwele ni mzuri kiafya?
Lishe bora ni ile yenye uwiano mzuri wa virutubisho na uwele ni moja ya nafaka bora zaidi ambayo siyo ya kukosa kwenye idadi ya bidhaa zilizopo jikoni kwako. Glycemic index hutumika kubainisha ikiwa nafaka fulani ni nzuri kwa afya au haifai sababu wakati mwingine ulaji wa nafaka unaweza kuathiri kiwango cha sukari mwilini. Kwa kuwa na kiwango cha Glysemic index cha 54, uwele umekuwa mshindi namba moja juu ya nafaka zingine kwenye eneo la afya duniani kote.
Mimi ni mjamzito, Je, naweza kutumia uwele?
Bila shaka. Unaweza kula uwele katika kipindi chote ukiwa mjamzito na huwezi kupatana na changamoto yoyote. Hata hivyo ni vema kumuona mtaalamu wako wa lishe kabla kuamua kutumia aina fulani ya chakula.
Je, uwele hauwafai watu wa namna gani?
Kama una tatizo la tezi ya shingo ni vema kujitenga na ulaji wa uwele. Vinginevyo pata ushauri na mwongozo wa lishe kutoka kwa wataalamu wako wa lishe.
Je, uwele una madini ya Chuma mengi?
Uwele una utitiri wa viinilishe na madini muhimu mwilini kama vile Madini ya chuma, Zinc, Folic Acid pamoja na beta Carotene ambavyo vinaweza kusaidia kutatua matatizo ya utapiamlo kwa urahisi zaidi
Je, ninafaa kuloweka uwele kabla ya kupika?
Naam. Loweka kwa muda usiopungua saa 12 ili kurahisisha umeng’enyaji wake.